Kirimi.bible

Kazi ya kutafsiri Biblia kwa Lugha ya Kirimi ilipofikia

Chama cha Biblia cha Tanzania kwa kushirikiana na Kanisa tunafanya kazi ya kutafsiri Biblia kwa Lugha ya Kirimi. Kazi hii inafanyika kwa ustadi mkubwa na kuzingatia kanuni na utalaam wa tafsiri ya Biblia kutoka muungano wa vyama vya Biblia Ulimwenguni (UBS).
Kwa mantiki hiyo hapa chini katika picha tunaona Dr.Samy Tioye mmoja wa watafsiri Bingwa wa Lugha kutoka UBS akiwa na watafsiri wa Lugha ya Kirimi katika kuangalia usahihi wa kazi na akiwaonyesha watafsiri aina mbalimbali za tafsiri za Biblia na namna zinavyoweza kutumika kusaidia tafsiri ya Biblia kwa Lugha ya Kirimi, Katika ofisi ya tafsiri ya Biblia kwa Lugha Kirimi Mkoani Singida.

Tunatamani mno kuueneza ujumbe wa habari njema nchini kote Tanzania. Naomba uungane nasi.

Kuhusu Lugha ya Kirimi

WARIMI:

Katika Mkoa wa Singida kuna Lugha kubwa mbili ambazo ni Kirimi (Nyaturu) na Kinyiramba na pia kuna Lugha ndogo ndogo kama vile Wanyisanzu, n.k.

Kirimi (Nyaturu) ni Lugha inayopatikana Mashariki, Kaskazini na Kusini mwa Mkoa wa Singida. Kwa upande wa Mashariki Warimi wanapakana na Wagogo (Dodoma), kwa upande wa Kaskazini Warimi wanapakana na Wadatoga na kwa upande wa kusini ni Wanyamwezi.

Ungana Nasi

Unaweza kujihusisha na Miradi ya Bibilia ya Kiswahili kwa kuchangia:
– Ujuzi wa Tafsiri:
Ikiwa ungependa kufanya kazi na sisi kwenye mradi kama mtafsiri tafadhali wasiliana na imwangota@biblesociety-tanzania.org
– Kuchangia na kuwa Muanachama
Ikiwa ungependa kuchangia upatikanaji wa Biblia kwa Watoto, Vijana na Wafungwa tafadhali wasiliana na smshana@biblesociety-tanzania.org au
Tuma Mchango wako kwenye namba hii ya M-PESA 890890 au piga 0765 530 892 kwa maelekezo zaidi.
– Kusambaza:
ikiwa ungependa kuwa muenezaji wa Neno la Mungu (Biblia) tafadhali wasiliana na ekamwela@biblesociety-tanzania.org

Zaidi juu yetu

Maombi yako na msaada kwa kazi yetu vinathaminiwa sana. Ikiwa ungependa kujua zaidi juu ya kazi za Chama cha Biblia cha Tanzania ambazo tunazifanya katika miradi mbali mbali basi tafadhali bonyeza hapa:

Unaweza pia kujua zaidi kwa kutembelea Chama cha Biblia cha Tanzania Makao Makuu Dodoma:
16 Hatibu / 9th Road, Madukani Area
P.O BOX 175, Dodoma – Tanzania
https://biblesociety-tanzania.org

Wasiliana Nasi

The Bible Society of Tanzania

16 Hatibu / 9th Road, Madukani Area.
P. O BOX 175, Dodoma – Tanzania.

Tel: +255-(026)-2324661
E-mail: info@biblesocietY-tanzania.org