Mochi.Bible

Kuhusu Lugha ya Kimochi

Kimochi ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wachagga, yaani ni lugha moja katika mnyororo wa lugha za Kichagga. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kimochi imehesabiwa kuwa watu 597,000.
Hii lugha inazungumzwa katika maeneo ya Kilimanjaro na Manyara.

Tunatamani mno kuueneza ujumbe wa habari njema nchini kote Tanzania. Naomba uungane nasi.

Uzinduzi wa Biblia ya Kimochi

Mkuu wa KKKT ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Fredrick Shoo, amewataka Wakristo kuitunza na kuindeleza lugha zao za asili kwani ndio msingi na urithi walio nao.

Askofu Dkt. Shoo aliyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Biblia ya lugha ya Kimochi (Kichagga cha Old Moshi), iliyofanyika katika Usharika wa Bethel Msaranga, iliyoambatana na kuweka wakfu eneo la ujenzi wa Kanisa la Mtaa huo.

 

Askofu Dkt. Shoo alisema watu wengi wamekuwa wakipuuzia lugha zao na kusema ni vyema kujifunza na kuziendeleza lugha zao za asili. Katika Uzinduzi huo wa Biblia, Katibu wa Chama cha Biblia cha Tanzania, Dkt. Alfred Kimonge alisema mbali na Uzinduzi wa Biblia hiyo bado wanakabiliwa na changamoto ikiwemo wenye lugha zao kutotilia maanani na kutozipa kipaumbele.

“wengine wameshajiwekea kuwa kuwasiliana kwa lugha za asili ni udhaifu, wapendwa si kweli kwamba lugha za asili ni udhaifu. Lugha ya asili ndio inajenga moyo wa mtu na ndio lugha mama kwa wote wanaoishi,” alisema.

Sasa, tuna Biblia kamili 12 za lugha za kienyeji ambazo zimetafsiriwa na nyingine 41 ni Biblia za Agano Jipya.

Kuna mengi katika Biblia yanayolisha nafsi yangu, mafundisho mengi sana. Katika Biblia tuna kila kitu. Biblia ya Kimochi katika Old Moshi inaniletea shangwe kubwa. Katika uzinduzi wa Biblia ya Kimochi hapo Moshi Kilimanjaro.

PICHA NA MATUKIO

Get involved

You can get involved in Swahili Bible Projects by contributing:
– Translation skills: if you would like to work with us on a project as a Translator please contact bkirimi@biblesocieties.org
– Donating
– Distributing

More about us

Your prayers and support for our work are greatly appreciated. If you would like to find out more about Bible Societies that do projects for Swahili speakers then please click here:

You can also find out more by visiting these Bible Societies:
https://www.unitedbiblesocieties.org/society/bible-society-of-tanzania/

Contact Us

Chama cha Biblia cha Tanzania

16 Hatibu / 9th Road, Madukani Area
P.O BOX 175, Dodoma -Tanzania

https://biblesociety-tanzania.org

Tel: +255-(026)-2324661
E-mail: info@biblesociety-tanzania.org

×

Hello!

Click one of our representatives below to chat on WhatsApp or send us an email to support@biblesociety-tanzania.org

× How can I help you?