Chama cha Biblia cha Tanzania

Kuhusu Lugha nchini Tanzania

Kiswahili ni lugha ya Taifa nchini Tanzania. Ni lugha yenye watumiaji wengi  ukilinganisha na lugha nyingine zinazozungumzwa nchini. Historia inaonyesha, Tanzania ni nchi yenye  makabila zaidi ya 125 yanayozungumza lugha tofauti tofauti. Kutokana na wingi wa makabila hayo,wapo watanzania hususani maeneo ya vijijini wasiojua Kiswahili na wanatumia lugha zao za asili katika kusoma na kuwasiliana. Chama cha Biblia kinalenga kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na Neno la Mungu kwa lugha yake na kwa bei anayoweza kuimudu. Katika Kuhakikisha hilo  kuna miradi 10 ya tafsiri iliyoanzishwa, katika lugha ya Kikaguru, Kiha, Kihehe, Kirimi, Kinyiramba, Chasu, Kinyamwezi, Kifipa, Kinyia na Kirombo.

Tumefahulu kuwa na Biblia kamili 13 za lugha mbali mbali hapa nchini; Ambazo ni Kimochi, Kivunjo, Kimachame, Kidatooga, Kimasai, Kikurya, Kihaya, Kigogo, Kisukuma, Kiiraq, Kiswahili, Kinyakyusa na Kimachame.

Usambazaji wa Biblia za Kiswahili Nchini Tanzania

Wananchi wengi Tanzania wanatumia lugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano nchini kote. Upatikanaji wa Biblia za Kiswahili katika mtandao utasaidia kuwafikia kwa urahisi na hivyo kuchangamana vizuri na Neno la Mungu.

Kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya teknolojia, Wananchi wengi wameunganishwa na mtandao, hasa walioko makazini na wanafunzi wa vyuoni, hivyo wanaweza kupata maandiko kwa urahisi.

Nunua Biblia ya Kiswahili

Kazi ya Tafsri katika Lugha zetu

Hapa Tanzania kuna makundi/makabila ya lugha hai 132. Hadi sasa kuanzia 1846 hadi 2021 Chama cha Biblia, kwa kushirikiana na Kanisa tumetafsiri Neno la Mungu katika makabila yafuatayo;
[wpdatatable id=1]

Njoo, Tutafakari pamoja.

Shirikiana Nasi.

Mkutano wa Wanachama 2022

Mkutano Mkuu wa Wanachama 2022

-Unaweza kushiriki na sisi kwa kuwa na mwanachama wa Chama cha Biblia cha Tanzania na mwanachama wa Biblia kwenye klabu ya kuchangia kila mwezi

Jiunge nasi ili kupata jarida letu la kila mwezi!

Utapokea habari kutoka Chama cha Biblia cha Tanzania

Kuhusu Chama Cha Biblia

Tunashukuru kwa sala na msaada wenu juu ya kazi zetu za Chama. Ikiwa ungependa kujua zaidi kuhusu Vyama Vya Biblia ambayo hufanya miradi kwa wasemaji wa Kiswahili basi tafadhali bonyeza hapa:
https://www.unitedbiblesocieties.org/society/bible-society-of-tanzania

Unaweza pia kujua zaidi kwa kutembelea Mashirika haya ya Biblia:
http://biblesociety-kenya.org/
http://biblesociety-uganda.org/
http://biblesociety-rwanda.org/

15 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. 16 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.

No content available for verse of the day!

1Yohana 2:15-16(SUV)
Subscribe for this Verse of the Day a
Loading
Verse of the day image

Wasiliana nasi

Chama cha Biblia cha Tanzania

16 Hatibu / 9th Road, Madukani Area
P.O BOX 175, Dodoma -Tanzania

https://biblesociety-tanzania.org

https://shop.biblesociety-tanzania.org

Tel: +255-(026)-2324661
E-mail: info@biblesociety-tanzania.org

Place Your Order Now || Weka Agizo lako Sasa

The Bible Society of Tanzania (BST) is registered as a non-profit inter confessional organisation registered as a Non-Governmental Organisation, Registration No. S05722 of 1970

CONTACT INFO

×

Hello!

Click one of our contacts below to chat on WhatsApp

× How can I help you?