Kiswahili ni lugha ya Taifa nchini Tanzania. Ni lugha yenye watumiaji wengi ukilinganisha na lugha nyingine zinazozungumzwa nchini. Historia inaonyesha, Tanzania ni nchi yenye makabila zaidi ya 125 yanayozungumza lugha tofauti tofauti. Kutokana na wingi wa makabila hayo,wapo watanzania hususani maeneo ya vijijini wasiojua Kiswahili na wanatumia lugha zao za asili katika kusoma na kuwasiliana. Chama cha Biblia kinalenga kuhakikisha kila mtanzania anafikiwa na Neno la Mungu kwa lugha yake na kwa bei anayoweza kuimudu. Katika Kuhakikisha hilo kuna miradi 9 ya tafsiri iliyoanzishwa, katika lugha ya Kikaguru , Kiha , Kihehe , Kirimi, Kinyiramba, Chasu, Kinyamwezi, Kifipa na Kinyia.
Tumefahulu kuwa na Biblia kamili 13 za lugha mbali mbali hapa nchini; Ambazo ni Kimochi, Kivunjo, Kimachame, Kidatooga, Kimasai, Kikurya, Kihaya, Kigogo, Kisukuma, Kiiraq, Kiswahili, Kinyakyusa na Kimachame.